Soma Biblia Kila Siku Julai 2023Mfano
“Wao” katika m.10 ni “walio hodari” (m.9). Wenye nguvu hawa hutumia fedha walizojaliwa na Mungu kwa kuvunja amri zake zinazowaonya wasiwadhulumu wadogo katika jamii. M.10 unasema,Wao humchukia yeye akemeaye langoni, nao humzira anenaye maneno ya adili.Hii ni picha kamili ya mienendo ya nyakati zetu. Wanyonge ni wahanga wasio na nguvu. Lakini Mungu bado anashauri akisema,Tafuteni mema, wala si mabaya, mpate kuishi, … yachukieni mabaya; yapendeni mema; mkaithibitishe haki langoni(m.14-15). Tangu wakati wa Amosi, Mungu hajakoma kutushauri. Tusipotii, hakika hasira ya Bwana itatutafuna. Lakini tukiithibitisha haki, “yamkini” Mungu atatufadhili. Zingatia Isa 1:18-20 jinsi Mungu anavyotualika akisema,Haya, njoni, tusemezane, asema Bwana. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu. Kama mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi; bali kama mkikataa na kuasi mtaangamizwa kwa upanga; maana kinywa cha Bwana kimenena haya.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Julai 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kuelewa somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Kutoka na Amosi Karibu kujiunga na mpango huu.
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/