Soma Biblia Kila Siku Julai 2023Mfano
Moyo huwa mdanganyifu kuliko vitu vyote(Yer 17:9). Waisraeli walidhani wanamfanyia Mungu ibada, lakini ukweli ni kwamba waabuduo ilivyoelezwa hawaugusi moyo wa Mungu. Ili wagundue, Mungu aliendelea kuwaita kwa njia ya adhabu na mapigo.Lakini hamkunirudia mimi, asema Bwana. Kauli hii imethibitishwa katika m.6-10 inayosema,Mimi nami nimewapa usafi wa meno katika miji yenu yote, na kutindikiwa na mkate mahali penu pote; lakini hamkunirudia mimi, asema Bwana. Tena nimeizuia mvua msiipate, ilipobaki miezi mitatu kabla ya mavuno; nami nimenyesha mvua juu ya mji mmoja, nikaizuia mvua isinyeshe juu ya mji mwingine; sehemu moja ilipata mvua, na sehemu isiyopata mvua ilikatika. Basi kutoka miji miwili mitatu walitanga-tanga kuendea mji mwingine wapate kunywa maji, wasipate ya kuwatosha; lakini hamkunirudia mimi, asema Bwana. Nami nimewapiga kwa ukavu na koga; wingi wa bustani zenu na mashamba yenu ya mizabibu, na mitini yenu na mizeituni yenu imeliwa na tunutu; Lakini hamkunirudia mimi, asema Bwana. Nimewapelekea tauni, kama tauni ya Misri; vijana wenu nimewaua kwa upanga, na farasi wenu nimewachukulia mbali; nami nimeupandisha uvundo wa matuo yenu na kuuingiza katika mianzi ya pua zenu; lakini hamkunirudia mimi, asema Bwana.Watakaoenenda bila kujutia mapigo hayo, watapotea. Watakaoyapima hayo kwa majuto na toba, huponywa. Zingatia maana yake kwako, Mungu akisema,Ujiweke tayari kuonana na Mungu wako(m.12).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Julai 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kuelewa somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Kutoka na Amosi Karibu kujiunga na mpango huu.
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/