Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Julai 2023Mfano

Soma Biblia Kila Siku Julai 2023

SIKU 17 YA 31

Historia ikiandikwa kwa usahihi, husaidia kuelewa tabia ya wanadamu. Tangu kale wanadamu wamekuwa waovu, na Mungu hakunyamaza kuonya na kuadhibu. Kwa hiyo tunajua Mungu anavyochukia mienendo mibovu. Hii ni hulka ya Mungu. Wadameski, Wafilisti na wakazi wa Tiro walipowadhulumu Waisraeli, Mungu alitamka hukumu kwao. Kwa Wafilisti anasema,Kwa makosa matatu ya Gaza, naam, kwa manne, sitaizuia adhabu yake isimpate; kwa sababu waliichukua katika hali ya kufungwa kabila nzima, wawatie katika mikono ya Edomu; lakini nitapeleka moto juu ya ukuta wa Gaza, nao utayateketeza majumba yake. Nami nitamkatilia mbali mwenyeji katika Ashdodi; na yeye aishikaye fimbo ya enzi katika Ashkeloni; nami nitaugeuza mkono wangu uwe juu ya Ekroni; na mabaki ya Wafilisti wataangamia, asema Bwana MUNGU (m.6-8). Ndiye Mlipa kisasi wa haki.Kisasi ni juu yangu mimi; mimi nitalipa, anena Bwana(Rum 12:19). Tujifunze kwambaasiwepo mtu awaoneaye wengine akidhani atakuwa salama.

siku 16siku 18

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Julai 2023

Soma Biblia Kila Siku Julai 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kuelewa somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Kutoka na Amosi Karibu kujiunga na mpango huu.

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/

Mipango inayo husiana