Soma Biblia Kila Siku Julai 2023Mfano
Kuacha kumshukuru Mungu na kumpa heshima kwa ajili ya wokovu wake ni ishara ya kutomwamini na kumpenda. Waisraeli walipokataa kumwamini, waliishia jangwani. Kwa kinywa cha mtunga Zaburi Mungu anasema wazi,Nikaapa kwa hasira yangu Wasiingie rahani mwangu(m.11). Kwetu sisi ni vivyo hivyo.Tukichagua kutompenda na kumwamini hakika hatutaurithi uzima wa milele. Ndivyo anavyosema katikaEbr 3:12-15,Angalieni, ndugu zangu, usiwe katika mmoja wenu moyo mbovu wa kutokuamini, kwa kujitenga na Mungu aliye hai. Lakini mwonyane kila siku, maadamu iitwapo leo; ili mmoja wenu asifanywe mgumu kwa udanganyifu wa dhambi. Kwa maana tumekuwa washirika wa Kristo, kama tukishikamana na mwanzo wa uthabiti wetu kwa nguvu mpaka mwisho; hapo inenwapo, Leo, kama mtaisikia sauti yake, Msifanye migumu mioyo yenu, Kama wakati wa kukasirisha. Tupone namna gani? Tutaokolewa kama tukizingatia jinsi zaburi inavyotuonya katika m.7b-8a:Ingekuwa heri leo msikie sauti yake! Msifanye migumu mioyo yenu. Zingatia na kufanya unavyoelezwa katika m.1-2 na 6:Njoni, tumwimbie Bwana, Tumfanyie shangwe mwamba wa wokovu wetu. Tuje mbele zake kwa shukrani, Tumfanyie shangwe kwa zaburi. ... Njoni, tuabudu, tusujudu, Tupige magoti mbele za Bwana aliyetuumba.Rudia kusoma mistari hiyo ukifanya unavyoambiwa!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Julai 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kuelewa somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Kutoka na Amosi Karibu kujiunga na mpango huu.
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/