Soma Biblia Kila Siku Julai 2023Mfano
Musa anapewa maagizo na BWANA juu ya wanaoruhusiwa kula pasaka. Asishiriki mtu asiye mmoja wa Waisraeli. Wageni wote ni lazima wapitie kanuni ya kutahiriwa kwanza. Hivyo watatakaswa na kustahilishwa kuwa mmoja wa Waisraeli. Sheria hiyo ni mfano kwetu nyakati hizi za ufuasi wa Kristo. Ubatizo ni tohara ya Kristo. Ndivyo tunavyosoma katika Kol 2:11,Katika yeye[Kristo]mmetahiriwa kwa tohara isiyofanyika kwa mikono, kwa kuuvua mwili wa nyama, kwa tohara ya Kristo. Yesu alifanywa pasaka yetu, na sote tuliobatizwa na kumwamini tumepewa uhuru wa kula mwili na kunywa damu yake Yesu. Yeye ndiye kafara ya dhambi. Hakuna sharti lingine.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Julai 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kuelewa somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Kutoka na Amosi Karibu kujiunga na mpango huu.
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/