Soma Biblia Kila Siku Julai 2023Mfano
Israeli na Yuda wameikataa sheria ya Mungu ambaye alijifunua kwao kwa upendo na uweza mwingi. Aliwatoa utumwani na kuwarithisha nchi ya Kanaani baada ya kuwaondoa wenyeji wake. Akawatukuza kwa kuwainulia manabii na wanadhiri. Lakini hawakuangalia wema huo, bali waliwaharibu watumishi hao pamoja na kufanya maovu tele.Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa cho chote apandacho mtu, ndicho atakachovuna(Gal 6:7). Wema wake kwetu ni sauti inayotuita tumpende na tumtii. Hayo ndiyo malipo yetu sahihi kwake.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Julai 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kuelewa somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Kutoka na Amosi Karibu kujiunga na mpango huu.
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/