Soma Biblia Kila Siku Julai 2023Mfano
Musa anawapa Waisraeli maelekezo juu ya kondoo wa pasaka: Watapaka damu yake kwenye vizingiti vya juu na miimo ya milango. Wasitoke nje usiku huo, maana BWANA atakapopita kuwapiga Wamisri, damu hiyo itahakikisha uponyaji wao. Jambo hili ni la kukumbuka milele, kwao na vizazi vyao. Watalishika hata watakapoingia kwenye nchi ya ahadi. Lilivyofanyika Misri ni maandalizi ya pasaka ya BWANA, Yesu alipotoa damu yake ya thamani badala ya damu ya kondoo.Basi, ndugu, ... tuna ujasiri wa kupaingia patakatifu kwa damu ya Yesu, njia ile aliyotuanzia iliyo mpya, iliyo hai, ipitayo katika pazia, yaani, mwili wake(Ebr 10:19-20). Kifo cha Yesu ni ukombozi wetu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Julai 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kuelewa somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Kutoka na Amosi Karibu kujiunga na mpango huu.
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/