Soma Biblia Kila Siku Julai 2023Mfano
Somohuweza kugawanyika katika sehemu tatu: Tangazo la kutoka utumwani Misri (m.1-3), maandalizi ya pigo la mwisho ambalo ni kifo cha mzaliwa wa kwanza wa Wamisri (m.4-8), na Farao kuendelea kushupaza moyo wake (m.9-10). Kupitia sehemu hizi Musa anawaandaa watu kuondoka. Mojawapo ya maandalizi ni kukusanya vitu vya thamani, yaanivyombo vya fedha, na vyombo vya dhahabu(m.2). Kwa njia hiyo unabii kwambakila mwanamke ataomba kwa jirani, na kwa huyo akaaye naye nyumbani, vyombo vya fedha, na vyombo vya dhahabu, na mavazi; nanyi mtawavika wana wenu na binti zenu(3:22) unatimia. Mungu anawapa Waisraeli fidia ya mateso yao. Tumwamini Mungu, maana anatengeneza njia hata ambapo tunafikiri hakuna njia.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Julai 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kuelewa somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Kutoka na Amosi Karibu kujiunga na mpango huu.
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/