Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Julai 2023Mfano

Soma Biblia Kila Siku Julai 2023

SIKU 10 YA 31

Musa aliagizwa kuinua mikono yake mbinguni, kukawa na giza nene lililofunika maeneo ya Wamisri kiasi cha hao kushindwa hata kusogea kwenda popote kwa siku tatu. Ili Mungu audhihirishe ulinzi wake, Waisraeli walikaa katika nuru kwenye makazi yao. Kwa mara nyingine Farao anatoa ruhusa kwa masharti yasiyokubalika, na Musa anasisitiza ni lazima kufuata maagizo ya BWANA kikamilifu, akisema,Ni lazima utupe mikononi mwetu na wanyama wa dhabihu na wa sadaka za kuteketezwa, ili tupate kumchinjia Bwana Mungu wetu dhabihu. Makundi yetu pia watakwenda pamoja nasi; hautasalia nyuma hata ukwato mmoja; kwa maana inampasa kutwaa katika hao tupate kumtumikia Bwana, Mungu wetu; nasi hatujui, hata tutakapofika huko, ni kitu gani ambacho kwa hicho inatupasa kumtumikia Bwana(m.25-26). Ghadhabu ya Farao inatishia kumwua Musa. Farao anaamuru,Nenda zako, ujiangalie, usinione uso tena; kwani siku hiyo utakayoniangalia uso wangu utakufa(m.28). Tukiwa katika Kristo, tupo nuruni, na mabaya hayatatupata. MaanaBwana ndiye mlinzi wako; Bwana ni uvuli mkono wako wa kuume. Jua halitakupiga mchana, Wala mwezi wakati wa usiku. Bwana atakulinda na mabaya yote, Atakulinda nafsi yako. Bwana atakulinda utokapo na uingiapo, Tangu sasa na hata milele(Zab 121:5-8).

siku 9siku 11

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Julai 2023

Soma Biblia Kila Siku Julai 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kuelewa somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Kutoka na Amosi Karibu kujiunga na mpango huu.

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/

Mipango inayo husiana