Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Julai 2023Mfano

Soma Biblia Kila Siku Julai 2023

SIKU 5 YA 31

Farao alipotenda kwa ulaghai, Musa alitumwa atoe taarifa ya pigo la tauni mbaya kwa mifugo yote ya Misri. Kama BWANA alivyosema Farao aliendelea kuufanya moyo wake kuwa mgumu. Alituma watu kuchunguza kama mifugo ya Waisraeli imepona.Na tazama, hapana mmoja aliyekufa katika wanyama wa wana wa Israeli. Lakini moyo wa Farao ulikuwa mzito, wala hakuwapa hao watu ruhusa waende zao(m.7). Tunadhihirishiwa kwamba ulinzi wa Mungu hauondoki kwa watu wake. Ni dhahiri pia kwamba Mungu habadilishi mpango alioweka kwa kulitimiza kusudi lake. Ndivyo Musa alivyomwambia Farao,Kesho Bwana atalifanya jambo hili katika nchi(m.5). Tunapotafuta kuisikiliza sauti ya Mungu tufuate kamili anayosema, maana twajua kwamba anachosema atafanya.

Andiko

siku 4siku 6

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Julai 2023

Soma Biblia Kila Siku Julai 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kuelewa somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Kutoka na Amosi Karibu kujiunga na mpango huu.

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/

Mipango inayo husiana