Soma Biblia Kila Siku Julai 2023Mfano
Angalia kwamba wakati huu wa pigo la nne Mungu anaweka mpaka kati ya watu wake na Wamisri, mainzi wajae nchini kote isipokuwa maeneo ya Waisraeli. Zingatia pia isivyowezekana kujadili uamuzi wa Mungu kama Farao alivyojaribu kuhusu kiwango cha ruhusa ambayo anataka kutoa kwa Waisraeli. Katika m.25 anawaambia Musa na Haruni,Endeni mkamtolee Mungu wenu dhabihundani ya nchi hii. Na katika m.28 anaendelea kusema,Mimi nitawapa ruhusa mwende, ili mmchinjie dhabihu Bwana, Mungu wenu, jangwani;lakini hamtakwenda mbali sana. Maagizo ya Bwana lazima yafuatwe kama yalivyoagizwa. Tuwe waangalifu kuyashika tusije tukashusha viwango vyake. Tuweke mioyoni mwetu jinsi Farao alivyoonywa“asitende kwa udanganyifu tena”(m.29).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Julai 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kuelewa somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Kutoka na Amosi Karibu kujiunga na mpango huu.
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/