Kuanza: Mwongozo Rahisi Wa Kuomba Kwa UjasiriMfano
Mafunzo Makuu ya Yesu kuhusu Maombi
Yesu hakufikiri kwamba tungejua kila kitu kuhusu maombi. Aliwafundisha kwa neema wafuasi Wake waliotaka kujifunza jinsi ya kuomba katika Mahubiri ya Mlimani, akisema:
" Bali wewe usalipo, ingia katika chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele za Baba yako aliye sirini. Na Baba yako aonaye sirini atakujazi. Nanyi mkiwa katika kusali, msipayuke-payuke, kama watu wa mataifa; maana wao hudhani ya kuwa watasikiwa kwa sababu ya maneno yao kuwa mengi. Basi msifanane na hao; maana Baba yenu anajua mnayohitaji kabla ninyi hamjamwomba.
Basi ninyi salini hivi:
Baba yetu uliye mbinguni,
Jina lako litukuzwe.
Ufalme wako uje.
Mapenzi yako yatimizwe
hapa duniani kama huko mbinguni.
Utupe leo riziki yetu.
Utusamehe deni zetu,
kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu.
Na usitutie majaribuni,
lakini utuokoe na yule mwovu."
Mathayo 6:6–13
Ona baadhi ya mambo ya kweli ambayo Yesu alitaja:
Maombi sio lazima yawe marefu au magumu.
Maombi hayapaswi kuwa maonyesho ya hadharani, bali ni kuwa na uhusiano wa karibu na Mungu.
Maombi yanakaribishwa na Mungu. Yeye anapenda kuitikia tunapokuja kwake.
Maombi ni fursa ya kumwabudu Mungu na kutambua ukuu wake.
Maombi yanaweza kujumuisha kuomba msamaha, kuomba riziki, na kutafuta mapenzi ya Mungu.
Maombi yanaendeleza Ufalme wa Mungu duniani!
Ujuzi wetu na ubunifu wetu hauna maana, kwa sababu hatuweki imani yetu katika nguvu ya maombi yetu. Tumaini letu liko katika nguvu za Mungu, ambaye anatupenda na anatusikiliza na kutenda tunapoomba. Hii ndiyo sababu sisi huomba.
"Maneno sahihi" au utaratibu fulani sio lengo kuu la maombi. Yesu ndiye.
Sala
Baba yetu uliye mbinguni, jina lako litukuzwe. Ufalme wako uje. Mapenzi yako yatimizwe,
hapa duniani kama huko mbinguni. Utupe leo riziki yetu. Utusamehe deni zetu,
kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu.Na usitutie majaribuni,
lakini utuokoe na yule mwovu."
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Maombi ni zawadi, fursa nzuri ya kuwa na uhusiano na Baba yetu wa Mbinguni. Katika mpango huu wa siku 6, tutatambua yale ambayo Yesu alitufundisha kuhusu maombi na kuhimizwa kuomba kwa mfululizo na ujasiri mkubwa.
More
Tungependa kuwashukuru Christine Caine - A21, Propel, CCM kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.propelwomen.org/