Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kuanza: Mwongozo Rahisi Wa Kuomba Kwa UjasiriMfano

Kuanza: Mwongozo Rahisi Wa Kuomba Kwa Ujasiri

SIKU 5 YA 6

Njia Sita za Kuomba

Ukifanya utafiti kwenye mtandao kuhusu "jinsi ya kuomba," utapata mamia, kama sio maelfu, ya maoni, mazoea, na kanuni kuhusu maombi. Hakuna njia moja inayofaa ya kuomba, lakini hapa kuna miongozo inayoweza kukusaidia:

Omba katika Nyakati Zilizoratibiwa na Zisizoratibiwa

Ni muhimu kuwa na nyakati zilizoratibiwa na Mungu na pia nyakati zisizopangwa. Maandiko hutuhimiza kuomba bila kukoma (1 Wathesalonike 5:17). Popote uwezapo, vyovyote uwezavyo, omba!


Omba Peke Yako na Pamoja na Wengine

Tunapokuwa na wakati mgumu kusikia sauti ya Mungu, ni muhimu kuwa na marafiki ambao wanaweza kuomba pamoja nasi. Katika Biblia, tunamwona Mungu akikutana na watu binafsi katika maombi (Mathayo 6:6), wanaposali pamoja (Mathayo 18:20), na katika ushirika kama kanisa (Matendo 2:42).


Omba Kimoyomoyo na kwa Sauti

Omba kwa sauti, hata unapoomba peke yako. Unaweza kuhisi kama ni mazungumzo halisi, na unaungana zaidi na maneno yako unapoyafikiria, kuyazungumza na kuyasikia.


Omba Kwa Akili na Mwili Wako

Katika Biblia, tunaona mifano ya watu wakiomba wakiwa wamelala kifudifudi, wakiwa wamepiga magoti, wakiwa wameketi, wakiwa wamesimama, au wakiwa wameinua mikono. Kubadili mkao wa mwili kunaweza kutusaidia kuwa macho na kuungana na Mungu katika maombi.


Omba kwa Maneno Yako Mwenyewe na ya Wengine

Maombi wakati mwingine ni mafuriko ya mawazo na matamanio yetu tunapoyaeleza kwa Baba; lakini katika historia ya kanisa, waumini pia wameomba maombi yaliyoandikwa na wengine (wakati mwingine huitwa liturujia). Kuomba Zaburi au Sala ya Bwana ni mifano ya hili katika Biblia.


Omba Unapopumua

Maombi yanayoitwa na wengi "maombi ya kupumua", ni maombi yaliyokusudiwa kusaidia kuzingatia maneno ya ukweli kutoka kwa Maandiko: moja unapovuta pumzi, na nyingine unaposhusha pumzi, na kumwacha Roho Mtakatifu ajaze mapengo kama vile alivyoahidi kufanya (Warumi 8:26).

Sala

“Ninaamini (vuta pumzi). Saidia kutokuamini kwangu (shusha pumzi)."
“Uko pamoja nami sasa hivi (vuta pumzi). Asante (shusha pumzi)."
“Ninahisi kuwa sionekani (vuta pumzi). Asante kwamba Wewe unaniona (shusha pumzi)."
“Uliufanya mwili wangu (vuta pumzi). Nitauheshimu na kuutunza (shusha pumzi)."
“Hii ni ngumu (vuta pumzi). Nitasubiri kuona mkono wako ndani yake, Bwana (shusha pumzi)."

siku 4siku 6

Kuhusu Mpango huu

Kuanza: Mwongozo Rahisi Wa Kuomba Kwa Ujasiri

Maombi ni zawadi, fursa nzuri ya kuwa na uhusiano na Baba yetu wa Mbinguni. Katika mpango huu wa siku 6, tutatambua yale ambayo Yesu alitufundisha kuhusu maombi na kuhimizwa kuomba kwa mfululizo na ujasiri mkubwa.

More

Tungependa kuwashukuru Christine Caine - A21, Propel, CCM kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.propelwomen.org/