Kuanza: Mwongozo Rahisi Wa Kuomba Kwa UjasiriMfano
Maombi Huimarisha Imani Yetu
Tunapoona mahitaji makubwa na fursa katika ulimwengu, tunaweza kushawishika kujificha au kufikiri tunapaswa kuhangaika ili kuyatatua. Lakini tunapaswa kuitikia kwa utiifu na imani na kufanya kile ambacho Yesu alituambia tufanye tunapokabiliwa na changamoto ya "mavuno ni mengi, lakini watendakazi ni wachache", na hiyo ni kuomba kwanza. Tunaomba kwa ujasiri na kwa bidii kwamba Bwana wa Mavuno atafanya yale aliyo ahidi: Kutuma wafanya kazi. Ili kutusukuma.
Maombi huachilia nguvu zake, uwepo wake, na utoaji wake katika maisha yetu.
Ni ajabu kwamba tunaweza hata kusema maneno haya, “Baba yetu,” kama tunavyoona katika Mathayo 6:9. Mungu ni mtakatifu na mwenye kushangaza katika kila njia, na bado yeye pia ni Baba yetu, ambaye anatualika kuzungumza naye na pia kukaribia kiti chake cha enzi cha neema (Waebrania 4:16). Mungu anatupenda kwa upendo wa milele - hivi kwamba alimtoa Mwanawe kwa ajili yetu (Yohana 3:16).
Tunamwomba Mungu kwa jina la Yesu, hatuombi nguvu fulani ya ulimwengu isiyo na hisia au isiyopendezwa. Anajua idadi ya nywele kichwani mwako. Alijua hatima yako kabla hujapumua kwa mara ya kwanza. Alikuchagua na kukuridhia. Hivyo ndivyo anavyokupenda, na ndiyo maana anakusikiliza kwa makini wakati unapoomba!
Tunapojitolea kuomba kwa ajili ya mavuno makubwa ya Ufalme, tukitaja mahitaji ya ulimwengu na yetu wenyewe, Mungu huimarisha imani yetu. Roho Wake anafanya kazi ndani yetu, kupitia kwetu, na kuelekea kwetu tunapoomba, akitukumbusha kwamba sisi ni zaidi ya waombaji watiifu mbele zake, sisi ni washirika wapendwa pamoja naye.
Sala
“Baba, asante kwa kunipenda na kunisikiliza ninapoomba.Asante kwa kujibu kwa nguvu kamilifu, wakati unaofaa na wema. Ninawataja mbele yako wale wasiokufahamu katika familia yangu na jamii na nakuomba utume watu maishani mwao ili wamtangaze Yesu kwao. Na nakuomba unitume kwa hekima na ujasiri popote utakaponiita kuomba au kuzungumza kuhusu yale uliyoyatenda. Amina."
Kuhusu Mpango huu
Maombi ni zawadi, fursa nzuri ya kuwa na uhusiano na Baba yetu wa Mbinguni. Katika mpango huu wa siku 6, tutatambua yale ambayo Yesu alitufundisha kuhusu maombi na kuhimizwa kuomba kwa mfululizo na ujasiri mkubwa.
More
Tungependa kuwashukuru Christine Caine - A21, Propel, CCM kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.propelwomen.org/