Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kuanza: Mwongozo Rahisi Wa Kuomba Kwa UjasiriMfano

Kuanza: Mwongozo Rahisi Wa Kuomba Kwa Ujasiri

SIKU 4 YA 6

Kusikia kutoka kwa Mungu

Hakuna kitu kama kusikia sauti ya Mungu. Njia moja ya kumsikia ni kupitia Neno lake. Warumi 10:17 inatuambia, imani huja kwa kusikia, na kusikia kwa Neno la Mungu (NKJV). Lakini kama tunataka kutembea kwa imani na si kwa kuona, ikiwa tunataka kusikia Neno la Mungu na kuona ahadi za Mungu zikitimizwa, basi ni lazima tuendelee kuomba na kuamini kwamba Mungu ana mengi zaidi ya kutuambia. Hapa kuna mambo machache ya kukusaidia:

Uwe Na Shauku, Hata Unaposubiri

Kitabu cha 1 Samweli sura ya 3 kinaeleza jinsi Samweli alivyojifunza kutii sauti ya Mungu. Hii inamaanisha nini kwetu? Kama Samweli, huenda tusiitambue sauti ya Mungu mwanzoni. Huenda ikachukua wakati, uvumilivu, na ushauri wa wengine kutusaidia kutambua kile tunachosikia. Msikilize kwa hamu.


Uwe na Pahali Pake

Katika Injili zote, tunamwona Yesu akijitenga na wanafunzi wake na umati ili kutafuta mahali pa faragha pa kuomba. Alifanya hivi kwa sababu ingawa alikuwa na yeye ni Mwana wa Mungu, pia alikuwa mwanadamu kamili. Alikabiliana na mapambano na vikwazo sawa na sisi, ndiyo maana alituonyesha kwa mfano umuhimu wa kutafuta mahali pa faragha ili kuomba. Vivyo hivyo, popote uwezapo, kwa njia yoyote uwezavyo, chukua wakati katika siku yako ili kutuliza akili na kuomba.


Vumilia Ndani Yake

Ukianza kuomba kila siku kwa mfululizo na bado unaona ni vigumu kusikia sauti ya Mungu, usikate tamaa. Endelea Kusonga Mbele. Endelea kuamini. Endelea kuomba. Endelea kujifunza Neno la Mungu ili wakati atakapozungumza, utajua kwamba ni Yeye! Katika Yeremia 33:3, Mungu anaahidi, "Niite, nami nitakuitikia, nami nitakuonesha mambo makubwa, magumu usiyoyajua" (CSB). Hiyo ni ahadi inayostahili kukumbukwa na kuvumilia ili kuona ikitimizwa!

Sala

“Mungu, nakusifu kwa sababu Wewe ni mwema na unastahili kusifiwa. Kutoka kizazi hadi kizazi na umri hadi umri, hubadiliki kamwe. Wewe ni mwaminifu kwa ahadi zako. Unastahimili katika upendo wako. Wewe ni mwaminifu katika Neno lako. Zungumza, Bwana, mtumishi wako anasikiliza. Amina!”

siku 3siku 5

Kuhusu Mpango huu

Kuanza: Mwongozo Rahisi Wa Kuomba Kwa Ujasiri

Maombi ni zawadi, fursa nzuri ya kuwa na uhusiano na Baba yetu wa Mbinguni. Katika mpango huu wa siku 6, tutatambua yale ambayo Yesu alitufundisha kuhusu maombi na kuhimizwa kuomba kwa mfululizo na ujasiri mkubwa.

More

Tungependa kuwashukuru Christine Caine - A21, Propel, CCM kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.propelwomen.org/

Mipango inayo husiana