Soma Biblia Kila Siku 03/2024Mfano
Makuhani katika Agano la Kale walipatanisha watu na Mungu kwa damu ya mwanakondoo; kazi iliyorudiwa tena na tena. Yesu ni Kuhani wetu Mkuu. Alifanya kazi hiyo mara moja tu, kwa kuutoa uhai wake, na damu yake kumwagika msalabani. Wateule wa Mungu walikuwa na mwili na damu, hivyo Shetani aliweza kuwatia hofu ya mauti. Yesu alitwaa mwili na damu ili amharibu ibilisi aliyekuwa na nguvu za mauti, na hivyo awakomboe wote na hofu ya mauti. Hili ni tangazo zuri kwa wale wanaomtegemea Yesu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 03/ 2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Machi pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Waebrania. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/