Soma Biblia Kila Siku 03/2024Mfano
Waisraeli waliifanya mioyo yao kuwa migumu. Hivyo wengi waliangamizwa njiani. Roho anawaonya watu wa Mungu akisema,Leo, kama mtaisikia sauti yake, msiifanye migumu mioyo yenu.Waisraeli walikataa kumwamini Mungu ingawa waliona makuu aliyowatendea. Baadaye katika Zab 95:8-11 Mungu anawaonya akiwakumbusha:Msifanye migumu mioyo yenu; Kama vile huko Meriba Kama siku ya Masa jangwani.Hapo waliponijaribu baba zenu, Wakanipima, wakayaona matendo yangu.Miaka arobaini nalihuzunika na kizazi kile, Nikasema, Hao ni watu waliopotoka mioyo, Hawakuzijua njia zangu.Nikaapa kwa hasira yangu Wasiingie rahani mwangu. Tusipomwachia Yesu maisha yetu ayatawale, hatutaingia mbinguni.Kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo(Mdo 4:12). Waisraeli walipomgomea Mungu aliapa kuwa hawataingia Kanaani. Tukiendeleza ugumu wa mioyo, hatutaingia mbinguni. Kwa hiyo tunahimizwa kuonyana na kuimarishana.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 03/ 2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Machi pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Waebrania. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/