Soma Biblia Kila Siku 03/2024Mfano
Wajibu wa Kuhani Mkuu ulikuwa kutoa dhabihu kwa ajili ya dhambi za watu wanaotubu, wapate kusamehewa dhambi zao. Sasa Makuhani Wakuu wa Agano la Kale walikuwa wenye dhambi hawa wenyewe. Kwa hiyo ilibidi kwanza watoe dhabibu kwa ajili ya dhambi zao wenyewe, ndipo waliweza kutoa kwa ajili ya wengine. Yesu aliteuliwa na Mungu kuwa Kuhani Mkuu. Zingatia Zab 110:4,Bwana ameapa, wala hataghairi, Ndiwe kuhani hata milele, kwa mfano wa Melkizedeki. Yesu hakutenda dhambi, kwa hiyo hakuhitaji kujitolea dhabihu, ila alitoa maisha yake kuwa dhabihu kwa ajili ya dhambi zetu sisi.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 03/ 2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Machi pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Waebrania. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/