Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 03/2024Mfano

Soma Biblia Kila Siku 03/2024

SIKU 18 YA 31

Mungu aliapa kwa nafsi yake kuthibitisha ahadi yake kwa Ibrahimu. Katika Mt 5:33-37 Yesu anaagiza tusiape ili kuthibitisha tusemayo:Mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiape uongo, ila mtimizie Bwana nyapo zako;lakini mimi nawaambia, Usiape kabisa; hata kwa mbingu, kwa maana ndicho kiti cha enzi cha Mungu;wala kwa nchi, kwa maana ndiyo pa kuwekea miguu yake; wala kwa Yerusalemu, kwa maana ndio mji wa Mfalme mkuu.Wala usiape kwa kichwa chako, maana huwezi kufanya unywele mmoja kuwa mweupe au mweusi.Bali maneno yenu yawe Ndiyo, ndiyo; Siyo, siyo; kwa kuwa yazidiyo hayo yatoka kwa yule mwovu.Mkristo awe mtu wa kusema kweli tu. Mungu hakuwa na haja ya kuapa ila ni kwa ajili ya udhaifu wa wanadamu. Ibrahimu alipewa ahadi ya kuirithi nchi, sisi Wakristo tumepewa ahadi ya kuingia mbinguni. Kwa hiyo tunaishi kwa tumaini la kufikia ahadi hiyo. Mungu hasemi uongo wala habadili ahadi yake. Tumaini hilo ni nanga ya kutusaidia tusiyumbe katika imani.

siku 17siku 19

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 03/2024

Soma Biblia Kila Siku 03/ 2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Machi pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Waebrania. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/