Soma Biblia Kila Siku 03/2024Mfano
Makuhani wa Agano la Kale walitoa dhabihu kwa ajili ya dhambi zao kwanza. Yesu hakuwa na dhambi kwa hiyo hakuhitaji kutoa dhabihu kwa ajili yake mwenyewe, bali kwa ajili ya wanadamu. Hivyo amekuwa kuhani wa agano jipya. Sifa zake ni nzuri sana: Mtakatifu, asiyekuwa na uovu, asiyekuwa na waa lolote, aliyetengwa na wakosaji, aliyekuwa juu kuliko mbingu, asiye na haja ya kutoa dhabihu kwa dhambi zake maana yeye hana dhambi. Yesu alitoa dhabihu ya nafsi yake kwa ajili ya wenye dhambi.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 03/ 2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Machi pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Waebrania. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/