Soma Biblia Kila Siku 03/2024Mfano
Chakula cha Bwana si kwa kumbukumbu ya mateso ya Yesu tu, bali pia ni tumaini la kuja kwake mara ya pili na tegemeo letu la kuurithi uzima wa milele. Ni kwa sababu tunampokea Yesu ambaye anasema,Mimi ndimi chakula cha uzima(Yn 6:48). Ni vema kushiriki, kwani tushirikipo twaonyesha ushirika wetu na Kristo, na kuwa tayari kuokolewa naye kwa njia ya msalaba. Twapokea mwili na damu ya Kristo kwa ajili ya msamaha wa dhambi zetu, kama Yesu mwenyewe alivyosema,Huu ndio mwili wangu! ... hii ndiyo damu yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi(Mt 26:26-28). Lakini ni vema kujihoji kwanza ili kushiriki kwetu kuwe baraka na si laana, maana tushirikipo twatangaza mauti yake msalabani.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 03/ 2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Machi pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Waebrania. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/