Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 03/2024Mfano

Soma Biblia Kila Siku 03/2024

SIKU 26 YA 31

Mimi sitalihalifu agano langu(m.34). Ndivyo Mungu anavyoahidi, na ndiyo sababu ya mtunga zaburi kuendelea kumsifu Mungu na kutafakari juu ya agano hilo alilolifanya na mtumishi wake Daudi. Mungu alipanua ufalme wa Daudi na kumpa ushidi dhidi ya maadui zake. Kama Mungu mwenyewe anavyosema katika m.19-21,Nimempa aliye hodari msaada, nimemtukuza aliyechaguliwa miongoni mwa watu. Nimemwona Daudi, mtumishi wangu, nimempaka mafuta yangu mtakatifu. Ambaye mkono wangu utakuwa thabiti kwake, na mkono wangu utamtia nguvu. Lakini ni wazi kwamba sehemu ya ahadi ya Mungu inamhusu mwingine, huyu atakayekuwamzaliwa wa kwanzawa Mungu, nakuwa juu sana kuliko wafalme wa dunia(m.27). Ndiye Kristo Yesu. Hivyo hata sisi tunaomwamini Yesu siku hizi tunahusika na ahadi ya Mungu katika m.29 na 36:Wazao wake nao nitawadumisha milele, na kiti chake cha enzi kama siku za mbingu. ... Wazao wake watadumu milele, na kiti chake kitakuwa kama jua mbele zangu.Mungu anaporudia ahadi yake ni kwa lengo la kusema kwamba utimilifu wake hautaweza kukosekana!

siku 25siku 27

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 03/2024

Soma Biblia Kila Siku 03/ 2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Machi pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Waebrania. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/