Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 03/2024Mfano

Soma Biblia Kila Siku 03/2024

SIKU 29 YA 31

Watumishi wa Mungu hupaswa kuwa tayari kupata mateso kwa ajili ya haki, ila Mungu anasema tusiogope,Nisikilizeni, ninyi mjuao haki, watu ambao mioyoni mwenu mna sheria yangu; msiogope matukano ya watu, wala msifadhaike kwa sababu ya dhihaka zao(51:7). Lakini katika somo hili la Ijumaa Kuu, mtumishi wa Bwana anateseka siyo kwa ajili ya haki tu, bali pia kwa ajili ya dhambi zetu sote. Anatoa maisha yake ili sisi tupate msamaha, tupone.Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona(m.5). Kifo chake mwenye haki kimetufanya sisi wenye dhambi kuwa na haki kwa kumwamini.Kwa maarifa yake mtumishi wangu mwenye haki atawafanya wengi kuwa wenye haki.Ni kwa sababuatayachukua maovu yao(m.11). M.12 ni utabiri juu ya ufufuo wa Yesu, na mamlaka na utukufu wake baada ya kifo chake kwa ajili ya dhambi za wanadamu. Mungu anasema,Nitamgawia sehemu pamoja na wakuu, naye atagawanya nyara pamoja nao walio hodari; kwa sababu alimwaga nafsi yake hata kufa, akahesabiwa pamoja na hao wakosao. Walakini alichukua dhambi za watu wengi, na kuwaombea wakosaji.

siku 28siku 30

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 03/2024

Soma Biblia Kila Siku 03/ 2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Machi pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Waebrania. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/