Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 03/2024Mfano

Soma Biblia Kila Siku 03/2024

SIKU 27 YA 31

Ee Bwana, hata lini? Utajificha hata milele? Ghadhabu yako itawaka kama moto?(m.46) Tunafanyaje hapo inapoonekana kwetu kana kwamba Mungu hatendi tena kama alivyoahidi, bali amejificha na fadhili zake hazipo? Je, Mungu ni mwanadamu hata asahau ahadi zake? Wengine wanaanza kumdhihaki mteule wa Mungu (m.50-51,Ee Bwana, ukumbuke wanavyosimangwa watumishi wako ... naam, wamezisimanga hatua za masihi wako). Lakini mtunga zaburi anamlilia Mungu, akitegemea mambo mawili: Watu wanapovunja sheria za Mungu atawaadhibu.Wakizihalifu amri zangu, wasiyashike maagizo yangu, basi, nitawarudi makosa yao kwa fimbo, na uovu wao kwa mapigo(m.31-32). Lakini agano la Mungu litadumu milele (m.28,Agano langu litafanyika amini kwake). Kwenye msingi huu mtunga zaburi anathubutu kumkumbusha Mungu,Zi wapi fadhili zako za kwanza?(m.49).

siku 26siku 28

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 03/2024

Soma Biblia Kila Siku 03/ 2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Machi pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Waebrania. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/