Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 03/2024Mfano

Soma Biblia Kila Siku 03/2024

SIKU 30 YA 31

Ukiwa na shida unafanyaje? Labda unatafuta ushauri kwa marafiki au kwenda kwa waganga wa kienyeji? Wapo watu wengi sana wanaopata masononeko ya moyoni. Kutokana na matatizo, baadhi yao hujinyonga na wengine hupatwa na magonjwa ya moyo, maana njia zao zilizotumika kutatua matatizo hayo si sahihi. Zaburi hii inaonyesha njia ya kutatua matatizo. Kama watumishi wa Mungu hatuna haja ya kuhangaika tunapopitia katika matatizo, bali tumtwishe Yesu huzuni na mizigo yetu naye atafanya. Yeye mwenyewe amesema,Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi(Mt 11:28-30).

siku 29siku 31

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 03/2024

Soma Biblia Kila Siku 03/ 2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Machi pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Waebrania. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/