Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 03/2024Mfano

Soma Biblia Kila Siku 03/2024

SIKU 22 YA 31

Katika Yesu Kristo sheria ya ukuhani wa kurithi imebatilishwa. Ile sheria haikuwa kamilifu, maana ilikuwa na mapungufu. Dhabihu ya upatanisho ilitolewa kila mwaka, tena ilikuwa ya mnyama. Yesu alitoa maisha yake, yakawa dhabihu ya mara moja tu kwa watu wote na wakati wote. Makuhani wale wa sheria ya Haruni walikuwa na ukomo, maana walikufa, na ikabidi wengine wachukue nafasi zao. Yesu yu hai milele. Ni Kuhani Mkuu wa milele. Tena ukuhani wake umewekwa kwa kiapo cha Mungu (m.21,Wale walifanywa makuhani pasipo kiapo, bali yeye [Yesu], pamoja na kiapo, kwa yeye aliyemwambia, Bwana ameapa wala hataghairi, Wewe u kuhani milele).

siku 21siku 23

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 03/2024

Soma Biblia Kila Siku 03/ 2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Machi pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Waebrania. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/