Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 03/2024Mfano

Soma Biblia Kila Siku 03/2024

SIKU 16 YA 31

Neno la leo linaonya watu wa Mungu walioonja neema ya wokovu, wakashiriki maisha ya toba na uongozi wa Roho Mtakatifu, na wakalijua Neno la Mungu, wasirudi nyuma na kuasi. Kufanya hivyo ni kupoteza nafasi yetu katika ufalme wa Mungu. Mtu akimkufuru Roho Mtakatifu hatasamehewa:Kila dhambi na kila neno la kufuru watasamehewa wanadamu, ila kwa kumkufuru Roho hawatasamehewa(Mt 12:31).Mtu atakayemkufuru Roho Mtakatifu hana msamaha hata milele; ila atakuwa ana dhambi ya milele(Mk 3:29). Roho Mtakatifu ni mwalimu wetu mkuu anayetufundisha Neno la Mungu. Ukimkataa Roho Mtakatifu, umemwacha yule ambaye angekuonyesha njia ya kumrudia Mungu, na kuliamini neno lake. Zingatia ushuhuda katika Zab 5:11,Wote wanaokukumbilia watafurahi, watapiga daima kelele za furaha. Kwa kuwa Wewe unawahifadhi, walipendao jina lako watakufurahia.

Andiko

siku 15siku 17

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 03/2024

Soma Biblia Kila Siku 03/ 2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Machi pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Waebrania. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/