Soma Biblia Kila Siku 03/2024Mfano
Yesu akiwa katika mwili alikuwa mcha Mungu, mtu wa maombi, mtiifu kwa Baba yake. Alisikilizwa maombi yake na dua zake kwa jinsi alivyokuwa mcha Mungu. Maisha yake yamekuwa sababu ya wokovu wetu. Katika Mt 1:21 ujumbe wa Mungu kwa Yusufu unasomeka: [Mariamu]atazaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu, maana, yeye ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao.Ujumbe huo ni sawa na m.9 unaosema:Naye alipokwisha kukamilishwa, akawa sababu ya wokovu wa milele kwa watu wote wanaomtii.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 03/ 2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Machi pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Waebrania. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/