Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 04/2025Mfano

Soma Biblia Kila Siku 04/2025

SIKU 14 YA 30

Katika 8:33 Haruni na wanawe wanaambiwa, “Msitoke nje mlangoni pa hema ya kukutania muda wa siku saba, hata siku za kuwekwa wakfu kwenu zitakapotimia.Sasa siku hizi za kuandaliwa zimekwisha, na Haruni anatayarisha sadaka na kuanza kazi yake ya kuzitoa. Katika siku hii ya nane alitoa aina zote za sadaka zilizotajwa katika Law 1-7, isipokuwa sadaka ya hatia. Ni hapo tu katika torati yote kwamba mwana-ng’ombe anatolewa sadaka. Huenda sababu ni jinsi Haruni alivyotengeneza ndama wa dhahabu. Katika Kut 32:4 imeelezwa kwambaakaitengeneza kwa patasi, akaifanya iwe sanamu ya ndama kwa kuiyeyusha; nao wakasema, Hiyo ndiyo miungu yako, Ee Israeli, iliyokutoa katika nchi ya Misri. Kilele cha siku hii ya kuanzisha ibada kinatokea Haruni anapowabariki watu na utukufu wa BWANA unatokea na kuteketeza sadaka ya kuteketezwa.

siku 13siku 15

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 04/2025

Soma Biblia Kila Siku 04/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Aprili pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Walawi, Luka na 2 Petro. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.somabiblia.or.tz