Soma Biblia Kila Siku 04/2025Mfano

Ni desturi kwa jamii nyingi za Kiafrika kualikana katika karamu ya chakula cha jioni, kama fursa ya kuonyesha upendo na undugu. Yesu na wanafunzi wake walipoila pasaka ya Kiyahudi, alianzisha Chakula cha Bwana. Karamu hii inaonyesha upendo wa Yesu kwao, tena kwetu tunaoshiriki Ushirika Mtakatifu katika ibada zetu. Ni chakula cha agano ambapo tunapokea mwili na damu ya Yesu kwa ukombozi wetu. Kutoshiriki katika karamu hii takatifu ni kujinyima nafasi ya kupokea uzima wa milele. Zingatia Yesu anavyoeleza katika Yn 6:54-55,Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu anao uzima wa milele; nami nitamfufua siku ya mwisho. Kwa maana mwili wangu ni chakula cha kweli, na damu yangu ni kinywaji cha kweli.
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 04/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Aprili pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Walawi, Luka na 2 Petro. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.somabiblia.or.tz