Soma Biblia Kila Siku 04/2025Mfano

Wanawake walikuwa wa kwanza kufika kaburini asubuhi na mapema. Walikuwa na nia nzuri ya kuupaka mwili wa Yesu manukato. Walikutana na habari njema kuwa Yesu amefufuka. Kikwazo kikubwa kwao kilikuwa ni jiwe kubwa lililowazuia wasiingie kaburini. Kumbe, walikuta jiwe limeondolewa, na Yesu yu hai. Kizuizi kikubwa kinachotuzuia tusikutane na Mungu ni dhambi. Kumbe, tunapotafuta kumwona Yesu mfufuka, tunakuta kwamba ameshaondoa kizuizi hicho alipokufa kwa ajili yetu. Habari hii njema yatuweka huru.
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 04/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Aprili pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Walawi, Luka na 2 Petro. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.somabiblia.or.tz