Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 04/2025Mfano

Soma Biblia Kila Siku 04/2025

SIKU 25 YA 30

Sababu moja ya Petro kuandika ni kwamba alijua kwamba karibuni atauawa kwa sababu ya kulikiri jina la Yesu.Najua kwamba kule kuwekea mbali maskani yangu kwaja upesi, kama Bwana wetu Yesu Kristo alivyonionyesha. Walakini nitajitahidi, kwamba kila wakati baada ya kufariki kwangu mpate kuyakumbuka mambo hayo(m.13-15). Kwa hiyo hachoki kuwakumbusha ukweli wa Yesu; anayoandika ni mausia yake.Nitakuwa tayari kuwakumbusha hayo siku zote, ijapokuwa mnayajua na kuthibitishwa katika kweli mliyo nayo(m.12). Leo anasisitiza mambo mawili kwa nguvu:1.Yeye kweli ni shahidi wa utukufu wa Yesu, kwa hiyo ujumbe aliotoa kwao ni wa kuaminika kabisa.Hatukufuata hadithi zilizotungwa kwa werevu, tulipowajulisha ninyi nguvu zake Bwana wetu Yesu Kristo na kuja kwake; bali tulikuwa tumeuona wenyewe ukuu wake. Maana alipata kwa Mungu Baba heshima na utukufu, hapo alipoletewa sauti iliyotoka katika utukufu mkuu, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye. Na sauti hiyo sisi tuliisikia ikitoka mbinguni tulipokuwa pamoja naye katika mlima ule mtakatifu(m.16-18).2.Maneno ya manabii ni imara sana. Wayaangalie kwa makini, maana nikama taa ing’aayo mahali penye giza.Ila yanaeleweka tu kwa ufasiri wa Roho Mtakatifu. Petro akiwaambia waliangalie neno la Mungu, anawakumbushakwamba hakuna unabii katika maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu fulani tu. Maana unabii haukuletwa po pote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu(m.19-21; ukitaka kusoma zaidi juu ya jambo hili, angalia Lk 24:44-49).

siku 24siku 26

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 04/2025

Soma Biblia Kila Siku 04/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Aprili pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Walawi, Luka na 2 Petro. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.somabiblia.or.tz