Soma Biblia Kila Siku 04/2025Mfano

Usia wa tatu wa Petro ni kuwaonya juu ya manabii wa uongo (m.1-3).Wengi watafuata ufisadi [au, uharibifu]wao; na kwa hao njia ya kweli itatukanwa(m.2). Lakini kama hukumu ya Mungu ilivyokuwepo siku za zamani,hata siku hizi ipo.Ndivyo Petro anavyoonesha katika m.3b-11! Na kama Mungu alivyowaokoa Nuhu na Lutu, hata siku hiziajua kuwaokoa watauwa na majaribu(m.9). Kwa matunda yaotutawatambua(ukipenda soma maneno yote ya Mt 7:15-23)! Tunda la kweli na la msingi ni upendo, wala si kutoa pepo au kutenda miujiza. Paulo anaeleza zaidi katika 1 Kor 13:1-7:Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo na upatu uvumao. Tena nijapokuwa na unabii, na kujua siri zote na maarifa yote, nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo, si kitu mimi. Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha maskini, tena nikijitoa mwili wangu niungue moto, kama sina upendo, hainifaidii kitu. Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni; haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya; haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli; huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote(soma pia Gal 5:22-26 ukipenda kujifunza zaidi).
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 04/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Aprili pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Walawi, Luka na 2 Petro. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.somabiblia.or.tz