Soma Biblia Kila Siku 04/2025Mfano

Mtume Petro anatukumbusha jambo alilofundisha katika barua yake ya kwanza, kwamba kama tumeokoka na utumwa wa Shetani na kuwa watoto wa Mungu, basi tuishi kama watoto wa Mungu!Tumetakaswa dhambi zetu za zamani(m.9) nakukirimiwa vitu vyote vipasavyo uzima na utauwa kwa kumjua Yesu(m.3). Kwa hiyo basi, tukazane kuishi maisha haya mapya! Pamoja na imani katika Yesu Kristo tumepewa pia mambo yale yaliyotajwa katika m.5-7, yaani,wema, maarifa, kiasi, saburi, utauwa, upendano wa ndugu na upendo. Rudia m.8-11 ukitafakari maana yake:Mambo hayo yakiwa kwenu na kujaa tele, yawafanya ninyi kuwa si wavivu wala si watu wasio na matunda, kwa kumjua Bwana wetu Yesu Kristo. Maana yeye asiyekuwa na hayo ni kipofu, hawezi kuona vitu vilivyo mbali, amesahau kule kutakaswa dhambi zake za zamani. Kwa hiyo ndugu, jitahidini zaidi kufanya imara kuitwa kwenu na uteule wenu; maana mkitenda hayo hamtajikwaa kamwe. Maana hivi mtaruzukiwa kwa ukarimu kuingia katika ufalme wa milele wa Bwana wetu, Mwokozi wetu Yesu Kristo.
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 04/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Aprili pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Walawi, Luka na 2 Petro. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.somabiblia.or.tz