Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 04/2025Mfano

Soma Biblia Kila Siku 04/2025

SIKU 27 YA 30

Manabii wa uongo hawatoki mbali. Hutokea kati kati ya kundi la waumini. Niwatu waliokwisha kuyakimbia machafu ya dunia kwa kumjua Bwana na Mwokozi Yesu Kristo ila wakanaswa tena na kushindwa(m.20). Mafundisho yaoyanafananana mafundisho ya Biblia, lakini ni tofauti. Mafundisho yao si bila roho. Yohana anatuambia,Msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu. Tufanye hivyokwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani,lakini si Roho wa Mungu aliyenena kupitia kwao, bali ni roho ya shetani (1 Yoh 4:1)! Tafakari pia ilivyoandikwa katika m.16:Punda, asiyeweza kusema, akinena kwa sauti ya kibinadamu, aliuzuiawazimuwa nabii yule. Na vilevile Paulo asemavyo katika 2 Kor 11:12-15:Nifanyalo nitalifanya, ili niwapinge hao watafutao nafasi wasipate nafasi; ili kwamba katika neno hilo wajisifialo waonekane kuwa kama sisi. Maana watu kama hao ni mitume wa uongo, watendao kazi kwa hila, wanaojigeuza wawe mfano wa mitume wa Kristo. Wala si ajabu. Maana Shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru. Basi si neno kubwa watumishi wake nao wakijigeuza wawe mfano wa watumishi wa haki, ambao mwisho wao utakuwa sawasawa na kazi zao!

siku 26siku 28

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 04/2025

Soma Biblia Kila Siku 04/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Aprili pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Walawi, Luka na 2 Petro. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.somabiblia.or.tz