Soma Biblia Kila Siku 04/2025Mfano

Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyokudhani kukawia, bali huvumilia kwenu, maanahapendi mtu ye yote apotee, bali wote wafikilie toba(m.9). Jambo linalozungumziwa hapa ni ahadi ya Yesu Kristo kuja mara ya pili duniani kwa nguvu na utukufu mwingi. Walikuwepo, na bado wapo wanaoulizaiko wapi ahadi ile ya kuja kwake?(m.4). Yesu mwenyewe alivyoeleza inaweza kutusaidia kujibu:Baada ya dhiki ya siku zile, jua litatiwa giza, na mwezi hautatoa mwanga wake, na nyota zitaanguka mbinguni, na nguvu za mbinguni zitatikisika; ndipo itakapoonekana ishara yake Mwana wa Adamu mbinguni; ndipo mataifa yote ya ulimwengu watakapoomboleza, nao watamwona Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya mbinguni pamoja na nguvu na utukufu mwingi. Naye atawatuma malaika zake pamoja na sauti kuu ya parapanda, nao watawakusanya wateule wake toka pepo nne, toka mwisho huu wa mbingu mpaka mwisho huu(Mt 24:29-31). Kumbuka pia maneno ya malaika wakati Yesu alipopaa mbinguni: [Wanafunzi wa Yesu]walipokuwa wakikaza macho mbinguni, yeye alipokuwa akienda zake, tazama, watu wawili wakasimama karibu nao, wenye nguo nyeupe, wakasema, Enyi watu wa Galilaya, mbona mmesimama mkitazama mbinguni? Huyu Yesu aliyechukuliwa kutoka kwenu kwenda juu mbinguni, atakuja jinsi iyo hiyo mlivyomwona akienda zake mbinguni(Mdo 1:9-11). Ndugu, sikiliza ujumbe wa Mungu kwako leo:hapendi mtu ye yote apotee!Hata wewe, hapendi upotee! Umepangiwa na Mungu kusamehewa dhambi zako kwa sababu ya kifo cha Yesu. Tafadhali, tubu leo!
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 04/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Aprili pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Walawi, Luka na 2 Petro. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.somabiblia.or.tz