Soma Biblia Kila Siku 04/2025Mfano

Shabaha ya barua hii ni:1.KuwakumbushaWakristo juu ya maneno (ahadi) ya Bwana kwa manabii. Petro anasema kwambatuna lile neno la unabii lililo imara zaidi, ambalo, mkiliangalia, kama taa ing'aayo mahali penye giza, mwafanya vyema, mpaka kutakapopambazuka, na nyota ya asubuhi kuzuka mioyoni mwenu(1:19).2.Kuwaonyajuu ya yale yanayotaka kuwaangusha kiimani. Wapenzi mkitangulia kujua hayo, jilindeni nafsi zenu, msije mkachukuliwa na kosa la hao wahalifu mkaanguka na kuuacha uthibitifu wenu(3:17).3.Kuwaagizawawe tayari kwa kuja kwa Bwana, hata kama atakawia.Vitu hivi vyote vitafumuliwa hivyo, imewapasa ninyi kuwa watu wa tabia gani katika mwenendo mtakatifu na utauwa, mkitazamia hata ije siku ile ya Mungu, na kuihimiza; ambayo katika hiyo mbingu zitafumuliwa zikiungua, na viumbe vya asili vitateketea na kuyeyuka(3:11-12)?Neno “kujua” ni la msingi katika somo la leo. Kwakumjua Mungu na Yesu Bwana wetu(1) tunazidi kuongezewa amani na neema (m.2); (2) tumekirimiwa vitu vyote vipasavyo uzima na utauwa (m.3); na (3)tumekirimiwa ahadi kubwa mno (m.4). Je, wewe msomaji, unamjua?
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 04/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Aprili pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Walawi, Luka na 2 Petro. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.somabiblia.or.tz