Soma Biblia Kila Siku 04/2025Mfano

Zaburi hii inaonyesha kwamba Mungu anapowabariki watu wake, hata watu wasiomjua hupata kumjua na kubarikiwa naye(m.1-3). Hali hii inalingana na ahadi ya Mungu kwa Ibrahimu katika Mwa 12:1-3:Bwana akamwambia Abramu, Toka wewe katika nchi yako, na jamaa zako, na nyumba ya baba yako, uende mpaka nchi nitakayokuonyesha; nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki, na kulikuza jina lako; nawe uwe baraka; nami nitawabariki wakubarikio, naye akulaaniye nitamlaani; na katika wewe jamaa zote za dunia watabarikiwa. Linganisha pia na ahadi ya Yesu katika Mt 5:14-16:Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji hauwezi kusitirika ukiwa juu ya mlima. Wala watu hawawashi taa na kuiweka chini ya pishi, bali juu ya kiango; nayo yawaangaza wote waliomo nyumbani. Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni. Vilevile katika Mt 24:14 Yesu anasema:Habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja. Ombikatikam.1 linalingana na baraka inayotolewa ibadani kanisani ambayo inapatikana katika Hes 6:24-27:Bwana akubarikie, na kukulinda; Bwana akuangazie nuru za uso wake, na kukufadhili; Bwana akuinulie uso wake, na kukupa amani. Ndivyo watakavyoweka jina langu juu ya wana wa Israeli; nami nitawabarikia. Zaidi ya ile nuru ambayo Waisraeli na Wakristo wameleta kwa mataifa, kuna unabii katika m.4-7 unaohusu ile hali itakayokuwepo Mungu atakapoumba mbingu mpya na nchi mpya.Mataifa na washangilie, naam, waimbe kwa furaha, naana kwa haki utawahukumu watu, na kuwaongoza mataifa walioko duniani. Watu na wakushukuru, Ee Mungu, watu wote na wakushukuru. Nchi imetoa mazao yake MUNGU, Mungu wetu, ametubariki. Mungu atatubariki sisi; miisho yote ya dunia itamcha Yeye!
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 04/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Aprili pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Walawi, Luka na 2 Petro. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.somabiblia.or.tz