1
Mathayo 12:36-37
Neno: Maandiko Matakatifu 2024
Lakini nawaambia, katika siku ya hukumu watu watatoa maelezo kuhusu kila neno walilonena lisilo la maana. Kwa maana kwa maneno yako utahesabiwa haki, na kwa maneno yako utahukumiwa.”
Linganisha
Chunguza Mathayo 12:36-37
2
Mathayo 12:34
Enyi uzao wa nyoka! Mnawezaje kunena mambo mema, wakati ninyi ni waovu? Kwa maana kinywa cha mtu huyanena yale yaliyoujaza moyo wake.
Chunguza Mathayo 12:34
3
Mathayo 12:35
Mtu mwema hutoa yaliyo mema kutoka hazina ya mambo mema yaliyohifadhiwa ndani yake, naye mtu mwovu hutoa yaliyo maovu kutoka hazina ya mambo maovu yaliyohifadhiwa ndani yake.
Chunguza Mathayo 12:35
4
Mathayo 12:31
Kwa hiyo nawaambia, kila dhambi na kufuru watu watasamehewa, lakini mtu atakayemkufuru Roho Mtakatifu wa Mungu hatasamehewa.
Chunguza Mathayo 12:31
5
Mathayo 12:33
“Ufanye mti kuwa mzuri, nayo matunda yake yatakuwa mazuri. Au ufanye mti kuwa mbaya, na matunda yake yatakuwa mabaya. Kwa maana mti hutambulika kwa matunda yake.
Chunguza Mathayo 12:33
Nyumbani
Bibilia
Mipango
Video