1
Mwanzo 25:23
Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza
Mwenyezi-Mungu akamwambia, “Mataifa mawili yamo tumboni mwako; makabila mawili yatakayozaliwa nawe, yatafarakana. Moja litakuwa lenye nguvu kuliko lingine; mkubwa atamtumikia mdogo.”
Linganisha
Chunguza Mwanzo 25:23
2
Mwanzo 25:30
Kwa hiyo akamwambia Yakobo, “Nafa njaa; tafadhali, nigawie chakula hicho chekundu nile.” (Ndiyo maana walimpanga jina Edomu yaani mwekundu).
Chunguza Mwanzo 25:30
3
Mwanzo 25:21
Rebeka alikuwa tasa, kwa hiyo Isaka akamwomba Mwenyezi-Mungu. Naye Mwenyezi-Mungu akakubali ombi lake, Rebeka akapata mimba.
Chunguza Mwanzo 25:21
4
Mwanzo 25:32-33
Esau akasema, “Sawa! Niko karibu kufa; haki yangu ya mzaliwa wa kwanza itanifaa nini?” Yakobo akamwambia, “Niapie kwanza.” Basi, Esau akamwapia na kumwuzia Yakobo haki yake ya mzaliwa wa kwanza.
Chunguza Mwanzo 25:32-33
5
Mwanzo 25:26
Wa pili alizaliwa akiwa amemshika Esau kisigino, hivyo wakampa jina Yakobo. Isaka alikuwa na umri wa miaka sitini wakati Esau na Yakobo walipozaliwa.
Chunguza Mwanzo 25:26
6
Mwanzo 25:28
Basi, Isaka akampenda Esau kwa sababu alipenda kula mawindo yake, lakini Rebeka akampenda Yakobo.
Chunguza Mwanzo 25:28
Nyumbani
Biblia
Mipango
Video