1
Kutoka 23:25-26
BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA
Mtanitumikia mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, nami nitawabariki kwa chakula na maji na kuyaondoa magonjwa kati yenu. Hakutakuwa na mwanamke yeyote atakayepoteza mimba wala kuwa tasa katika nchi yenu. Nami nitawajalia maisha marefu.
Linganisha
Chunguza Kutoka 23:25-26
2
Kutoka 23:20
“Tazameni, mimi namtuma malaika awatangulie safarini ili awalinde na kuwafikisha katika nchi niliyowatayarishia.
Chunguza Kutoka 23:20
3
Kutoka 23:22
Lakini mkimsikiliza kwa makini na kufanya yote asemayo, mimi nitakuwa adui wa adui zenu na mpinzani wa wapinzani wenu.
Chunguza Kutoka 23:22
4
Kutoka 23:2-3
Usifuate genge la watu kutenda uovu, wala usijumuike na genge la watu kutoa ushahidi mahakamani ili kupotosha haki. Usiwe na upendeleo katika kesi ya maskini.
Chunguza Kutoka 23:2-3
5
Kutoka 23:1
“Usitoe habari za uongo. Usishirikiane na mtu mwovu ili kuwa shahidi mbaya.
Chunguza Kutoka 23:1
Nyumbani
Biblia
Mipango
Video