1
Yakobo 1:2-3
Biblia Habari Njema
Ndugu zangu, muwe na furaha mnapopatwa na majaribu mbalimbali, kwani mwajua kwamba imani yenu ikisha stahimili, itawapatieni uvumilivu.
Linganisha
Chunguza Yakobo 1:2-3
2
Yakobo 1:5
Lakini kama mmoja wenu ametindikiwa hekima, basi, anapaswa kumwomba Mungu ambaye atampatia; kwani Mungu huwapa wote kwa wingi na kwa ukarimu.
Chunguza Yakobo 1:5
3
Yakobo 1:19
Ndugu zangu wapenzi, kumbukeni jambo hili! Kila mtu na awe mwepesi wa kusikia lakini si mwepesi wa kusema wala mwepesi wa kukasirika.
Chunguza Yakobo 1:19
4
Yakobo 1:4
Muwe na hakika kwamba uvumilivu wenu utawategemeza mpaka mwisho, mpate kuwa wakamilifu na watimilifu, bila kupungukiwa chochote.
Chunguza Yakobo 1:4
5
Yakobo 1:22
Msijidanganye wenyewe kwa kusikiliza tu neno lake, bali litekelezeni kwa vitendo.
Chunguza Yakobo 1:22
6
Yakobo 1:12
Heri mtu anayebaki mwaminifu katika majaribu, kwani akisha stahimili, atapewa tuzo la uhai ambalo Mungu aliwaahidi wale wanaompenda.
Chunguza Yakobo 1:12
7
Yakobo 1:17
Kila kipaji chema na kila zawadi kamilifu hutoka mbinguni; hutoka kwa Baba, Muumba wa mianga, ambaye habadiliki wala hana alama yoyote ya ugeugeu.
Chunguza Yakobo 1:17
8
Yakobo 1:23-24
Yeyote anayesikiliza hilo neno lakini halitekelezi, huyo ni kama mtu anayejiangalia sura yake mwenyewe katika kioo. Hujiangalia mwenyewe, kisha huenda zake, na mara husahau jinsi alivyo.
Chunguza Yakobo 1:23-24
9
Yakobo 1:27
Dini iliyo safi na isiyo na hitilafu mbele ya Mungu Baba ni hii: Kuwasaidia yatima na wajane katika shida zao, na kujilinda mwenyewe usichafuliwe na ulimwengu huu.
Chunguza Yakobo 1:27
10
Yakobo 1:13-14
Kama mtu akijaribiwa, asiseme: “Ninajaribiwa na Mungu.” Maana Mungu hawezi kujaribiwa na uovu, wala yeye hamjaribu mtu yeyote. Lakini mtu hujaribiwa anapovutwa na kunaswa na tamaa zake mbaya.
Chunguza Yakobo 1:13-14
11
Yakobo 1:9
Ndugu aliye maskini anapaswa kufurahi wakati Mungu anapomkweza
Chunguza Yakobo 1:9
Nyumbani
Biblia
Mipango
Video