Silaha za Mungu - Matendo ya MitumeMfano
Pambana na Giza
HADITHI YA BIBLIA – Paulo na Sila gerezani " Matendo 16:16-31 "
Hatupigani na wanadamu lakini tunapingana na shetani na ukuu wake wa giza. Shetani anapenda kusababisha kutokuelewana na anaweza kutumia watu kuumiza wengine, lakini lazima tukumbuke kila wakati kuwa vita vyetu ni dhidi yake! Ulimwengu wetu ni mahali palipojaa dhambi, na kama wanadamu, mara nyingi tunatenda dhambi dhidi ya wenzetu. Lakini lazima tukumbuke kutopigana dhidi yetu, kwa sababu tunapofanya hivyo tunakuwa tumeanguka katika mtego wa adui.
Mungu anapenda kila mtu, hata ingawa tunafanya makosa. Tunashukuru Mungu kwa huruma zake tunapofanya makosa, kwa hivyo tunapaswa pia kuwahurumia wengine. Wakati mwingine adui anapotosha maneno au matendo yetu, ili tukasirike zaidi. Walakini, Mungu anapenda kila mtu, na hivyo tunapaswa kupenda kila mtu.
Katika hadithi ya leo ya Bibilia kutoka kitabu cha Matendo, Paulo na Sila wanafungwa gerezani. Walinzi wanawatendea mabaya, ingawa hawajafanya chochote kibaya. Walakini, Mungu anapowapa njia ya kutoroka, hawalipizi kisasi kwa walinzi, badala yake wanawaonea huruma, na kumwongoza mlinzi na familia yake yote kukubali Bwana katika maisha yao! Paulo na Sila wangemlaumu mlinzi kwa uovu dhidi yao, lakini badala yake walikumbuka kwamba vita vyao vilikuwa dhidi ya shetani na sio dhidi ya walinzi.
Lazima tukumbuke tunapovaa Silaha ya Mungu, kupigana na giza ya kiroho na sio dhidi ya wanadamu wenzetu!
"Nachagua kupigana na adui, na sio watu walio karibu nami."
MASWALI:
1. Je, maneno haya yana maana gani? "nguvu, mamlaka, na nguvu, ambazo zinatawala ulimwengu huu wa giza na pepo mbaya za kiroho."
2. Je, ni mifano mingine ipi ambapo tumepigana na wanadamu badala ya ulimwengu wa giza?
3. Je, kwa nini Mungu alitaka tufahamu kuhusu Silaha ya Mungu?
4. Je, ni kitu gani kilichokuwa na uchungu kiliwatendekea Paulo na Sila kabla ya kutupwa gerezani?
5. Je, jibu kwa swali la mlinzi wa gereza, "Nifanye nini ili niokolewe?" lilikuwa gani?
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Kuvaa Vazi la Kivita la Mungu sio ibada ya maombi ya kufanya kila asubuhi lakini mtindo wa maisha tunaoweza kuanza tukiwa wadogo. Mpango huu wa kusoma ulioandikwa na Kristi Krauss unawaangazia mashujaa kutoka katika kitabu cha Matendo ya Mitume.
More
Tungependa kumshukuru Equip & Grow kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.childrenareimportant.com/swahili/armor/