Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Silaha za Mungu - Matendo ya MitumeMfano

Silaha za Mungu - Matendo ya Mitume

SIKU 7 YA 10

Ngao ya imani

HADITHI YA BIBLIA – Paulo na meli iliyovunjika " Matendo 27:21-37, 28:1 "

Leo tunajifunza kuhusu ngao ya imani, silaha yenye umuhimu kwa ajili ya kujilinda kwa sababu tunaweza kuizungusha na kujikinga na shambulio fulani. Bibilia inasema kwamba tunaweza kuitumia ili kujizuia mishale ya moto ya yule mwovu. Haisemi "ikiwa" mishale itakuja, lakini inasema "wakati" itakapokuja, tutakuwa na nguvu ya kujilinda. Ukweli ni kwamba adui anatuvamia kila wakati. Adui yako anataka kukuvuruga kwa kutumia mishale ya moto na kukutia hofu. Amebuni mkakati wake maalum kwa ajili yako. Amechambua mazoea yako, hofu yako ya kina na udhaifu wako, na analenga mishale yake katika maeneo hayo haswa.

Imani ni kumwamini Mungu na Neno lake, hata ingawa hatuwezi kuuona ufalme wake wa kiroho. Tunajua kuwa Mungu yuko ingawa hatuwezi kumwona, na hiyo ni imani mioyoni mwetu. Kwa sababu tunayo imani, tunaweza kushinda shambulio hili la maadui.

Katika hadithi ya leo ya Bibilia kutoka kitabu cha Matendo, Paulo alikuwa baharini wakati wa dhoruba kali, na Mungu akamwambia kwamba hakuna mtu atakayeangamia ndani ya meli kutokana na dhoruba hiyo! Paulo alichagua kuamini kuwa ni Mungu aliyekuwa amezungumza naye, ingawa hakuweza kumwona Mungu.

Inafurahisha kuona kwamba Paulo akiwaambia watu kile Mungu alisema, na answaambia wale chakula kikubwa ili kupata nguvu. Paulo hakumwamini Mungu tu, lakini alikuwa tayari kushiriki hadharani ujumbe wa Mungu na wengine na kuchukua hatua kulingana na ujumbe huo! Angeaibika sana ikiwa mtu angeangamia kutokana na kuanguka kwa meli.Wakati mwingine pia tunahitaji kutangaza hadharani Neno la Mungu, tukimwamini Yeye badala ya wanadamu.

Je, utachukua ngao yako ya imani na kuamini mambo usiyoyaona?

Hivi ndivyo utakavyoshinda dhidi ya adui na kuzima mishale yake ya moto!

"Nachagua kumwamini Mungu na kuwa na imani."

MASWALI :

1. Katika maisha halisi, "mishale ya moto ya yule mwovu" ni migani?

2. Je, ni mfano mgani maalum wa jinsi unavyoweza kukwepa mshale kwa kutumia ngao yako ya imani katika maisha halisi?

3. Je, unafanya nini ili kuhakikisha hautaondoka nyumbani bila imani yako?

4. Je, Paulo alikuwa akienda wapi alipokuwa safarini katika hadithi ya leo ya Bibilia? Kulikuwa na watu wangapi katika meli hiyo?

5. Je, Paulo alijuaje kwamba meli ingeharibika lakini hakuna mtu angeangamia kwa sababu ya dhoruba?

siku 6siku 8

Kuhusu Mpango huu

Silaha za Mungu - Matendo ya Mitume

Kuvaa Vazi la Kivita la Mungu sio ibada ya maombi ya kufanya kila asubuhi lakini mtindo wa maisha tunaoweza kuanza tukiwa wadogo. Mpango huu wa kusoma ulioandikwa na Kristi Krauss unawaangazia mashujaa kutoka katika kitabu cha Matendo ya Mitume.

More

Tungependa kumshukuru Equip & Grow kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.childrenareimportant.com/swahili/armor/