Silaha za Mungu - Matendo ya MitumeMfano
Helmeti ya wokovu
HADITHI YA BIBLIA – Kubadilika kwa Sauli " Matendo 9:1-19 "
Ni muhimu kuvaa helmeti zetu za wokovu kwa sababu inaweza kuwa hatari ikiwa tutagongwa kichwani. Je, tutahakikisha vipi kuwa tumevaa helmeti zetu? Biblia inaweka wazi kuwa wokovu wetu unategemea kazi iliyomalizika ya Yesu Kristo msalabani. Alipokufa kwa ajili ya dhambi zetu, alilipa gharama na akanunua wokovu wetu! Hatuwezi kuingia mbinguni kwa matendo mema, lakini kwa kumwamini Yesu Kristo tu, njia pekee ya wokuvu. Hatuhitaji kuwa na sherehe za maombi kila siku ili tuweze kuvaa helmeti zetu za wokovu.
Ikiwa tumemwamini Bwana Yesu Kristo kwa wokovu wetu, basi tumevaa helmeti zetu!
Mungu alimtokea Sauli kwa njia ya kimiujiza katika hadithi ya leo ya Bibilia kutoka kitabu cha Matendo. Sauli, ambaye baadaye anabadilika kuwa Paulo, alikuwa anawadhihaki na kuwatesa Wakristo. Siku moja akielekea Dameski, Yesu alimtokea Sauli kwa ghafla kama mwangaza kutoka mbinguni na Sauli akaanguka chini na kupoteza uwezo wa kuona. Siku tatu baadaye, Mungu alimtuma Mkristo ili kumponya na kumleta kwa Kristo.
Wiki hiyo Sauli alimwamini Yesu na akaokolewa! Unaweza kuvaa helmet yako ya wokovu leo, jinsi Paulo alivyofanya, ikiwa utaomba na kumwamini Bwana Yesu Kristo kwa wokovu wako.
Omba nami, “Bwana Yesu, leo nakubali kuwa mimi ni mwenye dhambi na nimekosa. Ninaamini kuwa ulikufa msalabani kwa ajili ya dhambi zangu na kwamba unaishi. Ninakubali moyoni mwangu leo uwe Bwana na Mwokozi wangu. Asante kwa kunipokea, kunipenda, na kunipa uzima wa milele na wewe mbinguni!"
"Nachagua kumtumaini Bwana Yesu kwa wokovu wangu."
MASWALI :
1. Je, unaweza kuwa na uhakika wa wokovu wako?
2. Je, unafikiria unaweza kupoteza wokovu wako?
3. Je, ni nini kilimfanyikia Sauli alipokuwa akiendesha farasi wake kwenda katika mji wa Dameski?
4. Je, Mungu alimwambia Anania wa Dameski nini?
5. Anania alimwambia Mungu nini? Je, nini hutendeka tunapomlalamikia Mungu?
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Kuvaa Vazi la Kivita la Mungu sio ibada ya maombi ya kufanya kila asubuhi lakini mtindo wa maisha tunaoweza kuanza tukiwa wadogo. Mpango huu wa kusoma ulioandikwa na Kristi Krauss unawaangazia mashujaa kutoka katika kitabu cha Matendo ya Mitume.
More
Tungependa kumshukuru Equip & Grow kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.childrenareimportant.com/swahili/armor/