Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Silaha za Mungu - Matendo ya MitumeMfano

Silaha za Mungu - Matendo ya Mitume

SIKU 6 YA 10

Viatu vya injili ya Amani

HADITHI YA BIBLIA – Filipo na Mhabeshi " Matendo 8:26-40 "

Sasa ni wakati wa kuvaa viatu vyetu ili tuwe tayari kupiha hatua! Hii inamaanisha kwamba tuko tayari kushiriki injili, au tuko tayari kutii wakati wowote, au tuko tayari KWENDA kufanya jambo sahihi.

Kile tunachovaa katika miguu yetu huamua udhabiti na uwezo wetu wa kusonga. Viatu vinaathiri jinsi tunaweza kutembea au kukimbia. Viatu vibaya vinaweza kuathiri uwezo wetu, kupunguza kasi yetu, na kutufanya tuondoke katika mstari wa mapigano. Askari asiye na viatu anaweza kujiingiza katika hatari kubwa.

Hatupaswi kuwa na wasiwasi wa mahali tunapoenda katika vita kwa sababu ya viatu vyetu. Viatu hutuwezesha tupige hatua bila uoga huku tukizingatia kamili vita vilivyo mbele yetu. Mwili wa Kristo umetumwa ili kutangaza habari njema ya Ufalme wa Mungu, ambayo itaeneza njia Yake ya amani ulimwenguni kote. Tunapovaa viatu vyetu, tunakuwa tayari kusonga, kueneza habari njema kwa wengine.

Hadithi ya Filipo kutoka kitabu cha Matendo ni hadithi nzuri inayoelezea kuhusu mtu aliye tayari kwenda kutangaza injili. Ghafla malaika anamwambia ainuke na kwenda, akimpa maelekezo fulani kuhusu barabara katika jiji. Anapofika, Bwana anamwambia akimbilie gari fulani. Filipo anamwuliza mtu huyo ikiwa anaelewa anachosoma, anaingia kwenye gari, kisha anaendelea kushiriki injili. Mhebeshi anaamua kumchagua Kristo na anasimamisha gari ili abatizwe papo hapo! Filipo alimbatiza, lakini walipotoka katika maji, Filipo akatoweka! Roho wa Bwana alimpeleka Filipo mahali pengine ili aendelee kuhubiri injili.

Hii ni hadithi ya ajabu sana ya mtu ambaye alikuwa tayari kwenda kuishiriki injili!

"Ninachagua kuwa na uhusiano mzuri na Mungu na kuwa tayari kumtumikia kila wakati."

MASWALI :

1. Je, ni hali gani ambayo unaweza kuhitajika kushiriki injili ghafla, bila kujiandaa mapema?

2. Je, ungefundisha somo gani ikiwa ingekulazimu uongoze darasa?

3. Je, tofauti ya injili ya "AMANI" na injili ya woga ni nini?

4. Je, Mhabeshi alimuuliza Filipo nini?

5. Mhabeshi alipoona maji, aliomba nini?

siku 5siku 7

Kuhusu Mpango huu

Silaha za Mungu - Matendo ya Mitume

Kuvaa Vazi la Kivita la Mungu sio ibada ya maombi ya kufanya kila asubuhi lakini mtindo wa maisha tunaoweza kuanza tukiwa wadogo. Mpango huu wa kusoma ulioandikwa na Kristi Krauss unawaangazia mashujaa kutoka katika kitabu cha Matendo ya Mitume.

More

Tungependa kumshukuru Equip & Grow kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.childrenareimportant.com/swahili/armor/