Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Silaha za Mungu - Matendo ya MitumeMfano

Silaha za Mungu - Matendo ya Mitume

SIKU 5 YA 10

Kinga ya Kifuani ya Haki

HADITHI YA BIBLIA – Kornelio " Matendo 10:9-23 "

Kipande kinachofuata cha Silaha ya Mungu kutoka kwa sura ya 6 ya Waefeso ni kinga ya kifuani ya haki. Haki ni kuonyesha tabia ya umungu, au kufanya kilicho sawa, kizuri na aminifu. Kitendo cha kuendelea kufanya haki mbele za Bwana ndicho kinachotunza kinga ya kifuani. Mungu anatuomba katika maandiko tuwe wenye busara na kufanya jambo sahihi. Tunapofanya hivyo, tunaweza kuwa na hakika kwamba tumevaa kinga ya kifuani, na kwamba mioyo yetu imelindwa kikamilifu wakati tuko vitani. Kuna jambo la muhimu sana kuhusu kinga ya kifuani, inafunika mioyo yetu ambayo ni chombo muhimu, lakini katika upande wa mbele tu. Tunapoivaa, tunaweza kujeruhiwa lakini bado tunaweza kuamka na kuendelea na vita. Walakini, tunahitaji kukambiliana na vita moja kwa moja kwa sababu kinga ya kifuani hufunika upande wa mbele. Haitaweza kutulinda ikiwa tumegeuka, tunapokimbia na kutoroka.

Je, tabia ya uungu na haki ni nini? Je, tunajuaje kama tunayo? Bibilia inasema kwamba Kornelio alikuwa mcha Mungu na aliyemwogopa Mungu na ambaye alitoa kwa ukarimu na alisali mara kwa mara. Bibilia pia inasema kwamba Wayahudi wote walimheshimu. Wengine watajua wakati wewe ni mwenye haki, kwa sababu kwa wakati inakuwa dhahiri kuona. Kornelio alikuwa amevaa kinga yake ya kifuani. Wakati huo, ilikuwa kinyume cha sheria kwa Wayahudi kushirikiana na watu wa mataifa mengine au hata kuwatembelea. (Matendo 10:28)

Mungu alituma maono kwa Petro ili aende kushiriki Injili na Kornelio. Kwa sababu Kornelio alikuwa mcha Mungu, Mungu alituma mtu kwake (hata dhidi ya sheria) ili kumwokoa yeye na familia yake yote!

"Nachagua kila wakati kufanya jambo sahihi."

MASWALI :

1. Je, ni katika hali gani za maisha yako ambapo umedhihirisha kwamba umevaa kinga ya kifuani ya haki na ni hali gani ambapo umeshindwa kuionyesha?

2. Fafanua jinsi unaweza danganya kuwa mwenye haki.

3. Je, ni katika hali gani ambapo unaweza kuchagua kutofanya chochote badala ya kufanya kitu kisha uaibike?

4. Je, Petro alienda kutembelea nyumba ya nani? Kwa nini hatua hio ilikuwa sio kawaida?

5. Je, ni kwa njia gani Kornelio alikuwa tofauti na wanaume wengine katika eneo hilo?

siku 4siku 6

Kuhusu Mpango huu

Silaha za Mungu - Matendo ya Mitume

Kuvaa Vazi la Kivita la Mungu sio ibada ya maombi ya kufanya kila asubuhi lakini mtindo wa maisha tunaoweza kuanza tukiwa wadogo. Mpango huu wa kusoma ulioandikwa na Kristi Krauss unawaangazia mashujaa kutoka katika kitabu cha Matendo ya Mitume.

More

Tungependa kumshukuru Equip & Grow kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.childrenareimportant.com/swahili/armor/