Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Silaha za Mungu - Matendo ya MitumeMfano

Silaha za Mungu - Matendo ya Mitume

SIKU 10 YA 10

Kuomba bila kukoma

HADITHI YA BIBLIA – Peter aachiliwa gerezani " Matendo 12:1-19 "

Maombi ni silaha ya pili ambayo tunaweza kutumia ili kumshambulia adui. Na pia yanaweza kutumika kama kinga. Kwa maombi tunaweza kupigana vita, kupokea hekima kutoka kwa Bwana kuhusu jinsi ya kuendelea, kuachilia malaika mbinguni kutupigania, na kuelewa vizuri adui yetu.

Katika hadithi ya leo ya bibilia, tunaona Petro akiwa gerezani wakati kanisa lote lilikuwa likimuombea.

Wakati wanaomba, Mungu anatuma malaika gerezani na kumwachilia Petro! Malaika anamwongoza nje ya gereza, kwenye barabara na Petro anarudi nyumbani ambapo ndugu na dada katika Kristo wanaomba. Walikuwa wanakataa kumfungulia mlango kwa sababu hawakuwa wana uhakika ni yeye!

Walikuwa wakiombea wokovu wake, lakini walishangaa kuona miujiza ikitendeka! Mara nyingi, wewe na mimi huwa tunaomba, lakini tunashangaa wakati Mungu anajibu maombi yetu na anapotusaidia.Anatuelekeza tuwe tunamwomba na anaahidi kutusaidia. Hii ni sehemu moja ya Silaha ambayo lazima utekeleze kila siku ikiwa unataka kuitumia kila siku.

Maombi hubadilisha mambo! Omba kila wakati katika vita vyako kwa sababu tunahitaji maombi katika vita leo zaidi ya jana.

"Nachagua kuomba kila wakati, nikikumbuka kuwa vita ni vya kiroho."

MASWALI :

1. Je, kwa nini maombi yamejumuishwa kama sehemu ya "Silaha ya Mungu"?

2. Je, ni mfano gani wa maombi ya kujilinda dhidi ya adui na ni mfano gani wa maombi ya kushambulia adui?

3. Ikiwa Mungu ana udhibiti wa kila kitu, kwa nini Anatuuliza tumwombe wakati tayari anajua kitakachotokea?

4. Je, ni silaha gani mbili za mashambulizi tunaweza kutumia?umia?

5. Je, ni nani aliyekuja mlangoni wakati Petro alibisha nyumbani kwa Mariamu?

Mpango huu wa kusoma umetolewa kutoka kwa mtaala wa watoto wa Equip & Grow, unaoangazia mashujaa kutoka kitabu cha Matendo ya Mitume. Furahia mpango huu ukiwa nyumbani, kisha ufanye mtaala kamili kanisani ukitumia vitabu vya wanafunzi, michezo, ufundi, nyimbo, mapambo na mengineyo!

https://www.childrenareimportant.com/swahili/armor/

siku 9

Kuhusu Mpango huu

Silaha za Mungu - Matendo ya Mitume

Kuvaa Vazi la Kivita la Mungu sio ibada ya maombi ya kufanya kila asubuhi lakini mtindo wa maisha tunaoweza kuanza tukiwa wadogo. Mpango huu wa kusoma ulioandikwa na Kristi Krauss unawaangazia mashujaa kutoka katika kitabu cha Matendo ya Mitume.

More

Tungependa kumshukuru Equip & Grow kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.childrenareimportant.com/swahili/armor/