Silaha za Mungu - Matendo ya MitumeMfano
Kuwa na Msimamo
HADITHI YA BIBLIA – Kifo cha Stefano " Matendo 6:8-15, 7:51-60 "
Tunapojifunza kuhusu Silaha ya Mungu na kitabu cha Matendo, ni muhimu kutambua kwamba tunaweka Silaha ya Mungu na kuitumia. Hauwezi kuomba ili uweze kuvaa mshipi wako wa ukweli. Unaposema ukweli kupitia kinywa wako, na kuamini ukweli wa Mungu moyoni mwako, hapo ndipo unapovaa mshipi wa ukweli.
Wala hauwezi kuomba ili kuchukua ngao yako ya imani. Unapoishi na imani, ukiamini kile Mungu anasema na sio kile wanachosema watu, basi inamaanisha umechukua ngao yako ya imani mikononi mwako na unaitumia kujilinda dhidi ya adui. Na vile vile unatumia kanuni hii ili kuwa na msimamo. Hauwezi kuomba vifungu fulani ili kuwa na msimamo. Unapomwamini Mungu na kukataa kukata tamaa, unapata msimamo.
Stefano ni mfano mzuri kwetu katika hadithi ya leo ya Bibilia kutoka kitabu cha Matendo. Alikuwa mtu mwadilifu na mwenye busara, ambaye alivaa Silaha yake kila wakati. Wakati upinzani wa kidini ulipomkabili, alisimama kidete na kile alichoamini, ingawa ilimaanisha kifo chake.
Viongozi wa dini walimkasirikia sana kwa kuhubiri kuhusu Yesu Kristo hivi kwamba walichochea umati wa watu ili watoe vurugu na mwishowe wakampiga Stefano kwa mawe. Katika hadithi hii yote ya Bibilia, Stefano alisimama kidete na kile alichokiamini, na hakubadilisha maoni yake kulingana na maoni ya umma.
Kama unaamini Mungu wako na upo tayari kuteswa kwa ajili ya hilo, simama wima, na usimame imara kama umevaa Silaha kamili ya Mungu!
"Nachagua kusimama kidete."
MASWALI :
1. Je, maisha ya mwanadamu yana mazuri na mabaya gani?
2. Je, ni lini tunahitaji kusimama dhidi ya Shetani?
3. Je, ni kitendo gani muhimu zaidi tunahitaji kufanya ili tuweze kusimama kidete?
4. Je, ni nani anayejulikana kuwa na uso kama wa malaika wakati anashtumiwa kwa uwongo?
5. Je, alisema nini kabla ya kufa kwake?
Kuhusu Mpango huu
Kuvaa Vazi la Kivita la Mungu sio ibada ya maombi ya kufanya kila asubuhi lakini mtindo wa maisha tunaoweza kuanza tukiwa wadogo. Mpango huu wa kusoma ulioandikwa na Kristi Krauss unawaangazia mashujaa kutoka katika kitabu cha Matendo ya Mitume.
More
Tungependa kumshukuru Equip & Grow kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.childrenareimportant.com/swahili/armor/