Silaha za Mungu - Matendo ya MitumeMfano
Upanga wa Roho
HADITHI YA BIBLIA – Petro ahubiria umati " Matendo 2:12-17, 22-30, 34-41 "
Upanga wa roho ni kipande cha kwanza cha Silaha ambayo ni silaha halisi, badala ya kifaa cha kujilinda. Hii inamaanisha kuwa tunaweza kumshambulia adui kwa kutumia upanga. "Upanga wa Roho" ni Bibilia, au Neno la Mungu. Ili uweze kutumia upanga wako vitani, unahitaji kufahamu Maandiko. Hii inamaanisha kusoma bibilia yako tena na tena na pia kukariri mafungu ya Bibilia.
Katika hadithi ya kweli ya leo kutoka kwenye kitabu cha Matendo, Petro anatumia maandiko wakati anahubiria umati wa watu. Kuna watu waliokuwa pale ambao hawakumwamini Mungu na wakaanza kumdhihaki. Petro alisimama na kuhubiria wale waliomdhihaki; hakuhubiri tu, lakini alitumia maandiko kupigana vita. Tunapokuwa tumekariri maandiko vizuri, tunaweza kuyatumia maishani wakati tunapohitaji.
Siku hiyo watu elfu tatu waliokolewa na kujiunga na kanisa hilo kwa sababu Petro alitumia mahubiri kutoka kwa Neno la Mungu! Ilikuwa baraka ya kufana! Petro alitumia upanga wake kwa ustadi kwa sababu alikuwa amekariri maandiko kwa ajili ya hali hii mahususi. Alipigana na adui kwa ustadi na akawaleta watu 3000 katika upande wa Bwana!
Jinsi unavyofahamu mafungu mengi ya biblia, ndivyo unavyokuwa hodari zaidi katika kutumia upanga wako. Tunaposoma Neno na kulikariri, Mungu anatuwezesha kulikumbuka tunapolihitaji. Je, unatumia vipi upanga wako?
"Nachagua kujifunza Neno la Mungu na kulitumia katika maisha yangu ya kila siku."
MASWALI :
1. Je, ni wakati gani unaweza kumshambulia adui?
2. Je, ni mfano gani unadhihirisha matumizi ya upanga katika maisha halisi?
3. Je, watu hutumia upanga wa roho kwa njia ipi isiyofaa?
4. Je, ni watu wangapi waliokoka kwa sababu ya mahubiri ya Petro katika Yerusalemu siku ya Pentekosti?
5. Je, Wakristo hawa wapya walifanya nini ili kuonyesha kuwa wangefuata Kristo?
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Kuvaa Vazi la Kivita la Mungu sio ibada ya maombi ya kufanya kila asubuhi lakini mtindo wa maisha tunaoweza kuanza tukiwa wadogo. Mpango huu wa kusoma ulioandikwa na Kristi Krauss unawaangazia mashujaa kutoka katika kitabu cha Matendo ya Mitume.
More
Tungependa kumshukuru Equip & Grow kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.childrenareimportant.com/swahili/armor/